المدة الزمنية 2:47

NHC YAPONGEZWA NA BODI YA WAKURUGENZI

135 مشاهدة
0
2
تم نشره في 2021/10/12

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa imewapongeza Menejimenti na Wafanyakazi wote wa NHC kwa kazi kubwa wanayofanya hususan katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa nyumba. Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 12/10/2021 eneo la Iyumbu na Mwenyekiti wa Bodi ya NHC Dkt. Sophia Kongela wakati akitoa majumuisho ya ziara hiyo. Kipekee Mwenyekiti huyo ameipongeza Timu ya Ujenzi ya NHC katika miradi hiyo kwa kufanya kazi usiku na mchana na kujenga nyumba bora. Amewataka waendelee kupambana kikamilifu ili kukamilisha mapema miradi ya Iyumbu na Chamwino na kuwezesha nguvu kazi ya miradi hiyo kwenda katika Mji wa Serikali wa Mtumba kushiriki katika ujenzi wa majengo ya Ofisi za Wizara ambazo Shirika sasa limepewa kandarasi ya miradi hiyo. Amewataka watendaji kuzingatia ubora katika ujenzi wa nyumba ili ziweze kuvutia wanunuzi na hata wapangaji wanaozihitaji. Akizungumzia nyumba hizo Mwenyekiti huyo na Bodi yake wamefurahishwa na utaratibu wa Shirika wa kuzingatia watumiaji mbalimbali wakiwepo walemavu. Aidha, ameihakikishia Serikali kuwa NHC itatekeleza miradi iliyopewa na Wizara mbalimbali za Serikali katika Mji wa Serikali wa Mtumba kwa ufanisi, ubora unaokubalika na kwa wakati. Amesema kuwa Bodi yake itaendelea kuliunga mkono Shirika la Nyumba la Taifa katika utekelezaji wa kazi zake na akasisitiza kuwa miradi yote inayotekelezwa na Shirika ni vizuri ikazingatia muda uliowekwa wa kuikamilisha.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 0