المدة الزمنية 2:52

Basi La Mwendokasi Lagongana Na Pikipiki, Wawili Wafariki

بواسطة JamiiForums
452 مشاهدة
0
3
تم نشره في 2021/09/09

DAR: BASI LA MWENDOKASI LAGONGANA NA PIKIPIKI, WAWILI WAFARIKI - Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumnne Muliro amesema Septemba 8, saa tatu usiku basi la mwendo kasi liligongana na pikipiki na kusababisha vifo vya watu wawili - Ajali hiyo ilitokea barabara ya mwendokasi eneo la Lumbumba kwenye taa za kuongoza magari. Chanzo cha ajali hiyo imetajwa kuwa ni dereva wa pikipiki kujaribu kupita wakati taa nyekundu imewaka - Waliofariki ni Sami Riyaz Khan (17), aliyekuwa dereva na abiria wake Patrick Chohan(16). Wito umetolewa kwa madereva wa pikipiki kutii sheria na kuvaa kofia ngumu

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 1